Katika du´aa ya Qunuut kuna sentesi ambayo inaulizwa mara nyingi ambayo maimamu wetu huisema wanapoomba du´aa:

هب المسيئين منا للمحسنين

”Wasamehe wakosefu katika sisi kwa wale wema.”

Maoni ya karibu zaidi ni kwamba ni kwa njia ya uombezi. Maana yake ni kwamba umati huu mkubwa miongoni mwao kuna wakosefu na wema. Kwa hivyo wafanye waovu waongozwe na wale wema kwa kumfanyia kwake uombezi. Ni kama kwamba imesemwa ´pokea uombezi wa wale wema wetu juu ya wale waovu wetu`.

Mwisho. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake, Maswahabah zake na watakaowafuata hadi siku ya Malipo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 20
  • Imechapishwa: 22/03/2024