´Ishaa haina Raatibah kabla yake

Swali: Ukifika wakati wa ´Ishaa na mtu akataka kuswali kabla yake kuna Sunnah?

Jibu: ´Ishaa haina Sunnah ya Raatibah kabla yake. Rawaatib ni Rak´ah kumi. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

“Nilihifadhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Rak´ah kumi; Rak´ah mbili kabla ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada yake,  Rak´ah mbili baada ya Maghrib nyumbani kwake, Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa nyumbani kwake na Rak´ah mbili kabla ya Subh.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/247)
  • Imechapishwa: 22/03/2024