Kumswalia Mtume kwa pamoja kila baada ya Rak´ah mbili za Tarawiyh

Kuhusu yale uliyoashiria kitendo cha baadhi ya waswaliji kila wanapomaliza kuswali Rak´ah mbili wananyanyua sauti zao juu kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Swalah ya Tarawiyh yenyewe kama yenyewe ni Sunnah kwa mujibu wa maneno na matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah amekufaradhishieni swawm ya Ramadhaan na nimekusunishieni kisimamo chake.”

Isitoshe aliiswali kwa mkusanyiko zile nyusiku mbili na tatu za mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhaan. Aidha aliiswali mara kadhaa katika lile kumi la mwisho kwa mkusanyiko. Kwa msemo mwingine kuiswali kwa mkusanyiko ndio bora zaidi kuliko mtu kuswali peke yake.

Hata hivyo mikusanyiko ya kupanga kwa ajili ya kufanya Dhikr na mfano wake kukiwemo kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada yake ni Bid´ah na haikuwekwa katika Shari´ah. Mtu anaweza pia kusema kwamba kuchukulia jambo hilo kuwa ni kawaida na kukusanyika kwalo ni jambo linalokinzana na yaliyowekwa katika Shari´ah. Ukiongezea baya zaidi ni kupaza sauti juu msikitini, jambo ambalo linakusanywa na matamshi mengine ya haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (2/246-247)
  • Imechapishwa: 22/03/2024