144. Kumsifu Mtume Muhammd kwa kupindukia ni haramu

Wakati waislamu wanapomsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sifa asizokuwa nazo, wanakuwa wamejifananisha na manaswara. Kwa hivyo jambo hilo linakatazwa kutokana na sababu mbili:

1 – Ni uwongo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mtukufu zaidi kutokana na kusifiwa kwa uwongo.

2 – Kufunga njia kwa kuchelea hilo lisiwapelekee katika yale yaliyowapelekea manaswara juu ya Mtume wao, kama kudai kuwa ni mungu na mfano wake. Licha ya Hadiyth hii na nyenginezo, waislamu wengi wametumbukia katika makatazo haya. Hayo yanathibitisha ukweli wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Hakika mtafuata nyayo za wale waliokuwa kabla yenu hatua kwa hatua, shubiri kwa shubiri, mpaka wakiingia shimo la mburukenge nanyi mtaingia. Wakasema: “E Mtume wa Allaah! Unamaanisha mayahudi na manaswara?” Akasema: “Kina nani wengine?”[1]

[1] al-Bukhaariy (4356) na Muslim (2669).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 200-201
  • Imechapishwa: 22/11/2023