145. Shirki katika mashairi ya ”al-Burdah”

Licha ya hayo mpaka hii leo tunawasikia baadhi wakimzungumzisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema:

Hakika katika ukarimu wako ni dunia na mali zake

na miongoni mwa elimu zako ni elimu ya Ubao na Kalamu

Huku ni kushirikisha katika baadhi ya sifa Zake Allaah (Ta´ala). Kama ambavo Allaah ni Mmoja katika uola na haki Yake ya kuabudiwa, basi vivyo hivyo ni Mmoja katika sifa Zake; hakuna kiumbe yeyote anayeshirikiana Naye, pasi na kujali namna atakavyokuwa mkubwa na utukufu atakaokuwa nao. Pindi Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomsikia msichana mmoja akiimba mashairi yasiyokuwa na hatia:

Mionogoni mwetu tuko na Mtume anayejua ya kesho

akamwambia: ”Yaache haya na sema yale uliyokuwa ukiyasema kabla.”[1]

Maneno ya msichana huyu hayawezi kulinganishwa na yale yanayoimbwa na baadhi ya waislamu kwa mamia ya miaka:

na miongoni mwa elimu zako ni elimu ya Ubao na Kalamu

Kwa mujibu wa watu hawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayajui yatayopitika kesho peke yake, bali anayajua yote yaliyokuweko na yote yatayokuweko yaliyoandikwa na Kalamu kwenye Ubao uliohifadhiwa. Yule ambaye atavisoma vitabu vya Suufiyyah basi ataona mengi katika maajabu haya.

[1] al-Bukhaariy na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 201
  • Imechapishwa: 22/11/2023