Watu pekee wanaotakiwa kutangamana nawe na kula chakula chako

Swali: Hadiyth inayosema:

“Usisuhubiane isipokuwa na muumini na wala asile chakula chako isipokuwa aliye mchaji.”

Jibu: Ni nzuri.

Swali: Ni vipi Hadiyth hii inatakiwa kufanyiwa kazi ikioanishwa na maandiko mengine kuhusiana na maudhui haya?

Jibu: Maana yake ni kwamba asiwafanye kuwa marafiki ilihali sio watu wazuri. Marafiki zake wawe wanaomcha Allaah na wema. Lakini jambo lenye kuzuka kama vile mgonjwa na mfano wake na chakula cha ghafla hayahusiani na maudhui haya. Pamoja na hivyo mtu asiwafanye marafiki watu wasiokuwa wema. Kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwakaribisha wageni wengi wakiwemo manaswara wa Najraan, waabudia mizimu na wengineo… wageni na jambo linalomzukia mtu ni mambo yenye hukumu nyingine. Au mtu anaweza kukumbana na wageni ambao akala nao au wafanya kazi ambao akala nao. Hilo halipelekei wakawa ni marafiki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23184/ما-معنى-حديث-لا-تصاحب-الا-مومنا
  • Imechapishwa: 22/11/2023