Swali: Amepatia ambaye anaingiza jambo la kuwaraddi Ahl-ul-Bi´dah na wahalifu katika usengenyi?

Jibu: Hapana, amekosea. Anayedhihirisha Bid´ah hana usengenyi. Anayedhihirisha dhambi hana usengenyi. Usengenyi ni kwa ambaye maneno yake yamefichikana na hakuyadhihirisha. Bi maana ameficha matendo yake mabaya. Lakini akiyatangaza haiwi usengenyi.

Usengenyi ni kule kumtaja kwa jambo ambalo hakulidhihirisha. Kuhusu kwa ambaye amedhihirisha maovu na madhambi hakuna usengenyi kwa yale aliyodhihirisha. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ

“Allaah hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule ambaye kadhulumiwa.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu wote ni wenye kusamehewa isipokuwa wenye kudhihirisha.”

Alisema wakati alipoingia bwana mmoja asiyekuwa na kheri:

“Mwache aingie. Ndugu mbaya aliyoje!”[2]

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu walipita na jeneza na wakalisifu ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Imewajibika.” Kisha kukapita jeneza lingine ambalo wakalisema vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Imewajibika.” Ndipo ´Umar akasema: “Ee Mtume wa Allaah! “Watu wamepita na jeneza na wakalisifu ambapo ukasema: “Imewajibika.” na wakapita na jeneza lingine ambalo wakalisema vibaya na wewe ukasema: “Imewajibika.” ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi. Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi. Nyinyi ni mashahidi wa Allaah juu ya ardhi.”[3]

Walimsifu vibaya kutokana na yale yaliyowadhihirikia na hakuwakemea kwa jambo hilo. Kwa hiyo ikafahamisha kuwa ambaye anadhihirisha shari hakuna usengenyi juu yake.

[1] 04:148

[2] Ahmad (6/38), al-Bukhaariy (6032) na Muslim (2591).

[3] Ameipokea al-Bukhaariy (1367) na Muslim (949).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23185/حكم-غيبة-من-اظهر-فسقا-او-بدعة
  • Imechapishwa: 22/11/2023