384 – Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka wakati wa baridi pindi majani yanaanguka. Akachukua tawi la mti mkavu, majani yake yakawa yanaanguka. Kisha akasema: “Ee Abu Dharr!” Nikasema: “Nakuitikia, ee Mtume wa Allaah!” Akasema:

“إنَّ العبدَ المسلمَ ليصلّي الصلاةَ يريد بها وجهَ الله، فَتَهافَتُ عنه ذنوبُه كما يتهافتُ هذا الورقُ عن هذه الشجرة

“Wakati mja muislamu anaposwali swalah huku akikusudia uso wa Allaah, yanaanguka madhambi yake kama ambavo majani haya yanavyoanguka kutoka kwenye mti huu.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/277)
  • Imechapishwa: 22/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy