143. Waislamu hawachupi mipaka kwa Mtume wao

Mambo mbalimbali:

1 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Msinisifu kwa kupindukia kama manaswara walivomsifu ´Iysaa bwana wa Maryam kwa kupindukia. Hakika si vyengine mimi ni mja wa Allaah.”[1]

[1] al-Bukhaariy (3445), at-Tirmidhiy katika ”ash-Shamaa-il al-Muhammadiyyah” (2/161), ad-Daarimiy (2/230), at-Twayaalisiy (25) na Ahmad (154, 164, 331 na 391).

al-Munaawiy amesema:

”Kupindukia ni kule kusifu kwa kupitiliza na kuchupa mipaka. Maana yake ni kwamba msivuke mipaka kwa kunisifu kwa kitu kisichokuwa cha uhalisia. Jambo hilo likawapelekea katika kufuru kama ambavo manaswara walivyokufuru pindi walipovuka mipaka katika kumsifu ´Iysaa (´alayhis-Salaam) na hatimaye wakaanza kumwabudu.”

Kisha akasema:

”Kufananisha pale (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema ”manaswara walivomsifu ´Iysaa bwana wa Maryam” kunakusudiwa pale walipodai kuwa ni mungu. Ni sahihi pia kusema kuwa kunakusudiwa yale yote yanayonasibishwa kwake yasiyokuwa sahihi, hivyo kujifananisha kunakuwa kumeenea zaidi.”

Hili ndio sahihi. Kwa sababu sisi tunatambua fika ya kwamba manaswara wamechupa mpaka juu ya ´Iysaa (´alayhis-Salaam) katika mambo mengi yasiyohusiana na madai yao ya kumfanya mungu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 200
  • Imechapishwa: 22/11/2023