383 – Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

الطُّهورُ شَطْرُ الإيمان، والحمدُ لله تملأُ الميزانَ، وسبحانَ الله والحمدُ لله تملآن -أو تملأ- ما بين السماءِ والأرضِ، والصلاةُ نُورٌ، والصدقةُ برهانٌ، والصبرُ ضِياءٌ، والقرآن حُجَّةٌ لك أو عليك

“Twahara ni nusu ya imani. Kusema “Himdi zote njema anastahiki Allaah (الحمد لله) kunajaza mizani, na kusema “Allaah ametakasika na mapungufu, na himdi zote njema anastahiki Allaah (سبحان الله والحمد لله) kunajaza yaliyomo kati ya mbingu na ardhi. Swalah ni nuru, swadaqah ni hoja, subira ni mwanga na Qur-aan ni ima hoja yako au dhidi yako. Kila mmoja ni mwenye kujipinda na kuiuza nafsi yake; ima akaiacha huru au akaiangamiza.”[1]

Ameipokea Muslim na wengineo.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/277)
  • Imechapishwa: 21/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy