Swali: Mtu akimtia mapungufu mwengine kwa kumwita kuwa ni Salafiy, Tabliyghiy, Ikhwaaniy na kadhalika kunahesabiwa ni usengenyi?

Jibu: Hapana. Kumtaja kwa namna hiyo sio usengenyi. Kumtaja kwa yale anayodhihirisha sio katika usengenyi. Yeye ndiye ambaye amejidhihirisha mwenyewe. Yeye ndiye ambaye amekiuka.

Swali: Kwa mfano kama kuna mtu amemwita mwenzake kuwa ni Salafiy kwa njia ya kumchezea shere. Anakusudia kuwa anaitakasa nafsi yake na kadhalika. Au kwa mfano akamwambia kuwa mtu fulani hamuhusu, kwamba mtu fulani ni Ikhwaaniy au kwamba ni Tabliyghiy.

Jibu: Ikiwa yuko na Bid´ah anatakiwa kunasihiwa nayo na kuelezwa sifa yake na kwamba ni katika Ahl-ul-Bid´ah. Hapana vibaya. Anatakiwa kuelezwa ili watu wajihadhari naye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23182/حكم-نسبة-شخص-لجماعة-معينة-للتنقيص-منه
  • Imechapishwa: 21/11/2023