Swali: Vipi kumsafirisha maiti kutoka mji moja kwenda mji mwingine?

Jibu: Bora mtu asifanye hivo. Maswahabah hawakuwa wakisafirisha. Anayekufa wanamzika mahali hapo. Muda wa kuwa kuna makaburi ya waislamu himdi zote njema anastahiki Allaah.

Swali: Hata kama aliacha wasia?

Jibu: Hata kama ameusia. Wasijikakame. Miongoni mwa Maswahabah kuna waliokufa Makkah, waliokufa Madiynah, kuna waliokufa Khaybar, kuna waliokufa Shaam, kuna waliokufa Yemen. Hawakuwa wakiwasafirisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23180/حكم-نقل-الجنازة-من-بلد-الى-بلد
  • Imechapishwa: 21/11/2023