14. Mahimizo ya Abu Haniyfah na matahadharisho yake

61- Amesema vilevile:

“Si ad-Dajjaal ambaye ninamukhofia zaidi juu yenu. Yatakuwepo mambo kutoka kwa wale wakubwa wenu. Hakika yule atakayekutana na kipindi hicho basi ashikamane na ile njia ya kwanza. Kwani hakika hii leo tunafuata Sunnah.”[1]

62- Ibn Mas´uud amesema:

“Yule ambaye katika nyinyi anataka kuigiza basi awaige Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwani wao walikuwa ndio watu bora wa Ummah huu. Nyoyo zao zilikuwa zikimcha Allaah zaidi, elimu yao ilikuwa imebobea na walikuwa wachache wa kujikalifisha. Allaah aliwachagua ili wasuhubiane na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wasimamishe dini Yake. Hivyo zitambueni fadhilah zao na zifuateni athari zao. Kwani hakika wao walikuwa katika njia iliyonyooka.”[2]

63- al-Hasan al-Baswriy alimtaja Mtume wa Allaahu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema:

“Walikuwa ndio watu bora wa Ummah huu na nyoyo zao zilikuwa zikimcha Allaah zaidi, elimu yao ilikuwa imebobea na walikuwa wachache wa kujikalifisha. Allaah aliwachagua ili wasuhubiane na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jishabihisheni na tabia na njia yao. Ninaapa kwa Mola wa Ka´bah kwamba wako katika njia iliyonyooka.”[3]

64- Ibraahiym amesema:

“Hakuna kitu kilichofikwa kwenu kutokamana na fadhilah zenu.”[4]

65- Hudhayfah amesema:

“Enyi wanachuoni! Shikamaneni na njia ya waliokuwa kabla yenu. Ninaapa kwa Allaah iwapo mtafanya hivo, basi mtafika mbali. Na mkiachana nayo basi badala yake mtaenda kuliani na kushotoni na mtapotea upotevu wa mbali kabisa.”[5]

66- Nuuh al-Jaamiy´ amesema:

“Nilisema kumwambia Abu Haniyfah: “Unasemaje juu ya yale yaliyozuliwa na watu kuhusu viungo na viwiliwili?” Akasema: “Maneno ya wanafalsafa. Lazimiana na mapokezi na njia ya Salaf.  Na tahadhari na kila kilichozuliwa, kwani hakika ni Bid´ah.”

[1] ad-Daarimiy (219) na al-Laalakaa-iy (107).

[2] Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih, uk. 419, na Mishkaat-ul-Maswaabiyh (193).

[3] Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (2/97).

[4] Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (2/97).

[5] Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (2/97).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 29-31
  • Imechapishwa: 18/12/2018