La tano: Ni wajibu kuheshimu Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuziadhimisha na kuzitukuza. Kwani ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Wahy kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

”Hatamki kwa matamanio yake. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” (an-Najm 53:03-04)

Kwa hivyo ni wajibu kuziheshimu Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kupunguza, kufanyia mzaha au kutukana kitu chochote katika hayo. Yule mwenye kufanya hivyo basi kwa hakika ameritadi kutoka katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 132
  • Imechapishwa: 18/12/2018