15. Kushikamana na Sunnah na Salaf

67- ´Aliy bin ´Asaakir al-Muqriy’ ametukhabarisha: al-Amiyn Abu Twaalib al-Yuusufiy ametuhadithia: Abu Ishaaq al-Barmakiy ametuhadithia: Abu Bakr bin Bukhayt ametuhadithia: ´Umar bin Muhammad al-Jawhariy ametukhabarisha: al-Athram ametuhadithia: ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Salamah ambaye amesema:”

“Lazimiana na Sunnah. Kwani – kwa idhini ya Allaah – ni kinga yako. Sunnah ni kinga kwa sababu itahuishwa na kufupika nayo. Imesuniwa na wale waliotambua kuteleza, makosa, upumbavu na ujikalifishaji ambayo hutokea pindi Sunnah itakhalifiwa. Tosheka na yale waliyotosheka nayo. Walisimama kutokana na elimu na yakini. Endapo kungekuwepo kitu bora ndani yake basi kingegunduliwa na kufuatwa na wale waliotangulia. Kwani wao ndio watangu wao. Kama ni kitu kilichozuliwa kilichotokea baada yao, basi kimezuliwa na ambaye hafuati njia yao na akawapa mgongo. Walizungumza kwa yenye kutosheleza na yenye kukata kiu. Yote yaliyo chini yao ni yenye mapungufu na yote yaliyo juu yao ni yenye kujichosha bure. Kuna ambao walipuuzia njia yao  ambapo wakawa ni wenye kutoheshimika, wengine wakataka zaidi ambapo wakachupa mipaka. Wao wako kati na kati, katika njia iliyonyooka.”

68- Abul-Fath Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy ametukhabarisha: Hamd bin Ahmad al-Haddaad ametuhadithia: Haafidhw Abu Nu´aym ametuhadithia kwa cheni ya wapokezi wake maneno mfano wa hayo kutoka kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz.

69- al-Awzaa´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Lazimiana na mapokezi ya wale waliotangulia japokuwa watu watakukataa. Na tahadhari na maoni ya watu japokuwa watakupambia nayo kwa maneno.”

70- Abu Ishaaq amesema: Nilimuuliza al-Awzaa´iy ambaye amesema:

“Isubirisheni nafsi yako juu ya Sunnah, simama pale waliposimama watu, sema kila walichokisema na jiepushe na kile walichojiepusha. Fuata njia ya watangu wako wema. Kwani kitakutosha kile kilichowatosha. Lau haya – yaani zile Bid´ah walizozua – yangelikuwa ni bora basi wangeliyagundua watangu wenu. Hakuna kitu kilichofikwa kwenu kutokamana na fadhilah zenu. Nao ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao Allaah amewachagua ili kusuhubiana na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akamtuma kwao na akawasifu kwake:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖتَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ndio wasifu wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili liwaghadhibishe makafiri. Allaah amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao maghfirah na ujira mkubwa.”[1]

71- Imaam Ahmad amesema:

“Msingi wa Sunnah kwetu ni kushikamana na yale waliyokuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaiga, kujiepusha na Bid´ah kwani hakika kila Bid´ah ni upotevu.”

72- ´Aliy al-Madiyniy amesema mfano wa hayo.

[1] 48:29

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 18/12/2018