139. Hatuulizi ”Vipi” wala ”Namna gani?”

38 – Wakiy´ bin al-Jarraah (127-197), mwanachuoni wa Kuufah.

184 – Ahmad bin Hanbal (Radhiya Allâhu ´anh) amesema: Wakiy´ ametuhadthia, kutoka kwa Israa’iyl, ambaye amesimulia Hadiyth:

”Pale Mola atakapokaa juu ya kiti… ”

Bwana mmoja aliyekuwa karibu na Wakiy’ akaanza kutetemeka ambapo Wakiy´ akakasirika na kusema: ”Tulikutana na al-A’mash na ath-Thawriy wakisimulia Hadiyth hizi na wala hawazipingi.’”
Hadithi hii imenukuliwa na Abu Hatim kutoka kwa Ahmad.

Ameipokea Abu Haatim kupitia kwa Ahmad[1].

185 – Yahya bin Yahyaa at-Tamiymiy amehadithia kuwa amemsikia Wakiy´ akisema:

”Yeyote anayeshuku kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah – kwa maana ya kwamba si kiumbe – ni kafiri. Na yeyote asiyeshuhudia kuwa Qur-aan imeteremshwa na si kiumbe ni kafiri kwa mujibu wa maafikiano ya wanazuoni wote.”[2]

186 – Ahmad bin ad-Dawraqiy amehadithia kuwa amemsikia Wakiy´ akisema:

”Tunajisalimisha Hadiyth hizi kama zilivyokuja. Hatuulizi ”Vipi” wala ”Namna gani?”[3]

Bi maana kama mfano wa Hadiyth inayosema ”Allaah atazibeba mbingu juu ya kidole… ” na ”Hakika nyoyo za wanadamu ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall).”

[1] Bali ameipokea Abdullaah katika “as-Sunnah”, uk. 70,  kutoka kwa baba yake Ahmad. Isitoshe Hadiyth ya Israa´iyl iliyotajwa si Swahiyh. Jengine ni kwamba ni masimulizi ya Swahabah na si maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[2] Cheni yake ya wapokezi iko katika usahihi wa hali ya juu na imesimuliwa na wengine kwa kifupi. Ameipokea ´Abdullaah, uk. 25, Abu Daawuud, uk. 266, na al-Bayhaqiy, uk. 249-250.

[3]Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea ´Abdullaah, uk. 55, ambaye amesema: Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 07/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy