40 – Wahb bin Jariyr (a.f.k 206), mmoa katika maimamu wa Baswrah.

188 – Muhammad bin Hammaad amesimulia ya kwamba amemsikia Wahb bin Jariyr akisema:

”Jihadharini na maoni ya Jahm. Kwani wanachojaribu ni kusema kwamba hakuna kitu chochote juu ya mbingu. Hakika hapana vyenginevyo isipokuwa ni wahy kutoka kwa shaytwaan, si vyenginevyo isipokuwa ni ukafiri.”[1]

41 – al-Asma´iy, mwanachuoni wa zama zake.

189 – Tumefikiwa na khabari kwamba mke wa Jahm amesema:

“Mke wa Jahm alifika wakati bwana mmoja alipomwambia kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi. Ndipo akasema: “Aliyefupika juu ya kilichofupika?” al-Asmaa´iy akasema: “Mwanamke huyu amekufuru kutokana na matamshi haya.”

[1] Masimulizi haya yamesahihishwa na Ibn-ul-Qayyim katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 85, ambaye amesema kwamba ”Haafidhw Muhammad bin ´Uthmaan ameisahihisha katika kijitabu chake cha ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 159
  • Imechapishwa: 07/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy