42 – al-Khaliyl bin Ahmad (a.f.k >160), kiongozi wa lugha ya kiarabu.

Muhammad bin al-Husayn amesema: al-Mu´aafaa bin Zakariyyaa ametuzindua: Muhammad bin Abiyl-Azhar ametuhadithia: az-Zubayr bin Bakkaar ametuhadithia: an-Nadhwr bin Shumayl ametuhadithia: al-Khaliyl bin Ahmad amenihadithia:

“Nilimwendea Abu Rabi’ah al-Araabiy, ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu wajuzi zaidi ninayemjua, alipokuwa juu ya paa lake. Alipotuona alitusalimia kwa ishara na akasema: “Inukeni (استووا).” Hatukujua alimaanisha nini, ambapo mzee aliyekuwa naye akasema: “Anakuambia muinuke.” al-Khaliyl amesema: ”Hiyo ndio asili ya maneno Yake (Ta´ala):

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi… ”[1][2]

Kwa maana ya kwamba akawa juu na kuinuka.”

190 – Muhammad bin al-Jahm amesema: Yahyaa bin Ziyaad bin al-Farraa’ amesema:

”Wakati wa Aayah:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi… ”

Ibn ´Abbaas alisema: ”Akapanda.” Ni kama unaposema kumwambia mtu: ”Alikuwa ameketi chini, kisha aka اسْتَوَى na kusimama.” Yote hayo ni sahihi kwa mujibu wa kiarabu.”

Ameipoke al-Bayhaqiy[3].

[1] 41:11

[2] Mtunzi amesema: ”Ahmad bin Abiyl-Khayr ametuzindua, kutoka kwa Yahyaa bin Buush: Abul-Mu´izz bin Kaadish ametukhabarisha: Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia…

Simjui huyu Muhammad bin Abiyl-Azhar, Muhammad bin al-Husayn wala Yahyaa bin Buush. Ahmad bin Abiyl-Khayr anaitwa Abul- ´Abbaas Ahmad bin Abiyl-Khayr Salaamah bin Ibraahiym ad-Dimashqiy al-Haddaad, kama ilivyotajwa katika “Mu´jam-ul-Muswannaf al-Latwiyf” (2/204). Kwa mujibu wa wasifu wake katika “ash-Shadhaaraat”, alifariki mwaka wa 678.

[3] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/310).

Cheni ya wapokezi kwenda hadi kwa al-Farraa’ haina neno. Haafidhw Ibn Hajar aliandika wasifu wa Muhammad bin al-Jahm bin Haaruun as-Simmariy al-Baswriy na akasimulia wenye kuhifadhi kadhaa madhubuti kutoka kwake na kusema:

”Sijui kujeruhiwa kwake.”  (Lisaan-ul-Miyzaan)

Kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika “al-Mushtabih” kwamba alikuwa ”mwenye kutambulika”.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 160
  • Imechapishwa: 07/01/2025
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy