Kwa ajili hiyo walikuwa wakichukia kusalimia kwa mkono, ameyasema hayo ´Atwaa’ bin Abiy Rabaah, kama yalivyotajwa na ”al-Adab al-Mufrad”, uk. 146, ya al-Bukhaariy, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Imekuja katika ”Fath-ul-Baariy” ya kwamba an-Nawawiy amesema:

”Makatazo ya kutoa salamu kwa kuashiria kunamkusudia yule ambaye ana uwezo wa kusalimia kwa kutamka na kwa njia iliyowekwa katika Shari´ah. Vinginevyo ni jambo linakubalika kwa mujibu wa Shari´ah kuitikia namna hiyo kwa yule ambaye atakuwa ameshughulishwa na jambo, kama vile anayeswali, aliye mbali, bubu na kiziwi.”

Hadiyth hii ni yenye kuenea na inawakusanya, mbali na wale waliotangulia kuvuliwa, anayetoa salamu kwa kuashiria na kwa kutamka au ambaye anaashiria peke yake, kitendo ambacho ndio kibaya zaidi kwa sababu kimekusanya kati ya kuiacha Sunnah ambayo ni kutamka salamu na pia kujifananisha na makafiri.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 193
  • Imechapishwa: 20/11/2023