2 – ash-Shurayd bin Shariyk ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinipitia na mimi nimekaa namna hii. Nilikuwa nimeweka mkono wangu wa kushoto nyuma ya mgongo wangu na nikauegemea. Akasema: ”Unakaa mkao wa wale walioghadhibikiwa?”[1]

[1] Abu Daawuud, al-Haakim na Ahmad (4/388). al-Haakim amesema kuwa cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Bali ni kwa mujibu wa  sharti za al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 196-197
  • Imechapishwa: 20/11/2023