Swali: Je, imethibiti kuwa ardhi haili miili ya mashahidi?

Jibu: Sijui jambo hilo. Hilo limepokelewa juu ya Mitume ya kwamba Allaah ameiharamishia ardhi kula miili ya Mitume. Lakini linaweza kutokea kwa baadhi ya waja wema hali ya kuwa ni heshima kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Haidhuru ikiwa ardhi itakula mwili wake. Kila mtu:

مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ ٰ

“Kutoka humo [ardhini] Tumekuumbeni na katika hiyo [ardhi] tutakurudisheni.”[1]

Mwanadamu wote atateketea isipokuwa kifupa kilicho kwenye uti wa mgongo wake (عَجْبُ الذَّنَبِ). Mtu ataumbwa tena kutokana na kijimfupa hicho siku ya Qiyaamah.

[1] 20:55

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23176/هل-تاكل-الارض-اجساد-الشهداء
  • Imechapishwa: 20/11/2023