Maana ya hakuna kinachorudisha nyuma makadirio isipokuwa du´aa

Swali: Tunaomba utuwekee wazi suala la makadirio kufungamana na du´aa.

Jibu: Hakuna kinachorudisha nyuma makadirio isipokuwa du´aa, maana yake ni kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameandika kila kitu. Baadhi ya mambo yanaweza kufungamana na matendo ya mja kwa njia ya kwamba akawepo mtu ambaye amekadiriwa kutokana na du´aa yake kuoa kwake, amekadiriwa kutokana na matendo yake mema kuhiji, kuswali na kutoa swadaqah. Kwa msemo mwingine kuna makadirio sampuli mbili:

1 – Ambayo haikufungamana na kitu. Kwa mfano kifo na mfano wake. Hii hakuna njia ya kuiepuka.

2 – Ambayo imefungamana. Fulani utarefushwa umri wake kwa sababu atawaunga ndugu zake. Allaah amemwandikia jambo hilo. Mtu huyu anawepesishiwa kwa kile alichoumbiwa kwacho katika kuwaunga jamaa na kutoa swadaqah, jambo ambalo linapelekea kuishi maisha marefu na kuongozwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Fanyeni matendo. Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kuwepesishiwa kile alichoumbiwa.”[1]

Wenye furaha watafanyiwa wepesi matendo ya wenye furaha. Wala khasara watafanyiwa wepesi matendo ya wala khasara. Mambo yamefungamana na makadirio yake.

[1] al-Bukhaariy (4945) na Muslim (2647) kupitia kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/ما-معنى-لا-يرد-القدر-الا-الدعاء
  • Imechapishwa: 20/11/2023