Adabu desturi:

1 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msisalimie salamu ya mayahudi. Salamu yao ni kwa kichwa, mkono na ishara.”[1]

[1] Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Ameipokea an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi nzuri.”

Huenda iko katika ”as-Sunan al-Kubraa” au katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah”. Kisha nikachapisha hii kwa nambari 430. Ndani yake Abuz-Zubayr hakutaja amesikia kutoka kwa nani. Tazama ”as-Swahiyhah” (1783). al-Haythamiy ametaja Hadiyth mfano wake kisha akasema:

”Ameipokea Abu Ya´laa na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw”. Wanaume wa Abu Ya´laa ni wenye kuaminika.” (Majma´-uz-Zawaa’id (8/38))

Inatiliwa nguvu na Hadiyth aliyopokea at-Tirmidhiy kupitia kwa Ibn Lahiy´ah, kutoka kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Si katika sisi yule mwenye kujifananisha na wasiokuwa sisi. Msijifananishe na mayahudi wala manaswara. Mayahudi wanasalimia kwa kuashiria kwa vidole, manaswara wanasalimia kwa kuashiria kwa mkono.”

at-Tirmidhiy amesema:

”Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu.” (3/386)

Ibn Lahiy´ah amedhoofishwa kutokana na kumbukumbu yake. Hata hivyo Hadiyth yake inatiliwa nguvu na Hadiyth ya kabla yake. Tazama Hadiyth inayofuata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 193
  • Imechapishwa: 20/11/2023