381 – Handhwalah al-Kaatib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

مَن حافظ على الصلواتِ الخمسِ؛ ركوعِهنَّ، وسجودِهنَّ، ومواقيتِهنَّ، وعلم أنهنَّ حقٌّ مِن عندِ اللهِ؛ دخل الجنّةَ، أو قال: وَجَبَتْ له الجنّةُ، أو قال: حَرُم على النار

“Yule mwenye kuhifadhi swalah tano, Rukuu´ zake, Sujuud zake na nyakati zake na akatambua kuwa ni haki kutoka kwa Allaah, basi ataingia Peponi.” Au alisema: “Itamthubutukia kwake Pepo.” Au alisema: “Moto kwake utakuwa ni haramu.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri. Wasimulizi wake ni wasimulizi wa Swahiyh.

[1] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/276)
  • Imechapishwa: 19/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy