Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Baada ya amri akataja sababu inayohusiana na sababu. Hiyo ikafahamisha kuwa kujitofautisha na waabudia moto ni jambo lililokusudiwa na Shari´ah. Kujitofautisha ndio sababu ilioko katika hukumu hiyo, sababu nyingine ya hukumu hiyo au angalau kwa uchache sehemu yake. Ijapo udhahiri ni kwamba hiyo ni sababu iliyokamilika. Ndio maana Salaf walipofahamu machukizo ya kujifananisha na waabudia moto katika jambo hili na mengine, wakachukizwa na mambo mengine vilevile ambayo ni katika mambo ya waabudia moto ambayo hayakutamkwa waziwazi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Marwaziy amesema:

”Nilimuuliza Abu ´Abdillaah – bi maana Ahmad bin Hanbal – kuhusu kunyoa shingo. Akajibu: ”Ni katika matendo ya waabudia moto; na yeyote atakayejifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

al-Khallaal amesimulia kwamba al-Mu´tamir bin Sulaymaan at-Tamiymiy ambaye amesema:

”Alikuwa baba yangu anapokata nywele zake basi hanyoi shingo yake. Anapoulizwa sababu ya hilo, hujibu kwa kusema kwamba hapendi kujifananisha na wasiokuwa waarabu.”

Wakati fulani Salaf wanatoa sababu ya machukizo kwa kujifananisha na watu wa Kitabu, na wakati mwingine kwa kujifananisha na wasiokuwa waarabu. Sababu zote mbili zimetamkwa waziwazi katika Sunnah ingawa mkweli na mwenye kusadikishwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikhabarisha waziwazi ya kwamba yatatokea yote mawili.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 187
  • Imechapishwa: 15/11/2023