6 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia tena kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mayahudi na manaswara hawapaki rangi; hivyo jitofautisheni nao.”[1]

[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ahmad (2/240, 260, 309 na 401).

ash-Shawkaaniy amesema:

”Hadiyth inafahamisha ni kwa nini imewekwa katika Shari´ah kuzipaka rangi mvi, nayo ni kujitofautisha na mayahudi na manaswara. Kwa ajili hiyo kuzipaka rangi ni jambo lililokokotezwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitilia mkazo kujitofautisha na watu wa Kitabu na akiamrisha jambo hilo. Salaf walijipinda juu ya Sunnah hii. Ndio maana utawaona wanahistoria pindi wanapowaelezea watu basi hutaja kama walikuwa wakipaka rangi au hawapaki. Ibn-ul-Jawziy amesema: ”Maswahabah wengi na wanafunzi wao walikuwa wakijipaka rangi. Ahmad bin Hanbal alimuona bwana mmoja amezipaka rangi ndevu zake akasema: ”Namuona mtu ambaye anaihuisha Sunnah iliyokufa.” Akafurahishwa naye wakati alipomuona amezipaka rangi ndevu zake.” (Nayl-ul-Awtwaar (1/105)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 187-188
  • Imechapishwa: 15/11/2023