130. Masuala yanayohusiana na kuwatumia makafiri

Suala la nne: Inajuzu kwa waislamu kuwatumia makafiri katika mambo asiyoweza yeyote kuyafanya vizuri isipokuwa wao tu. Inajuzu kwetu kustafidi kutoka katika uzowefu wao ambao hakuna awezaye isipokuwa wao tu au wao ndio wasanifu na wajuzi zaidi. Katika hali hiyo inafaa kuwatumia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuajiri Ibn Arayqitw amuonyeshe njia. Mtu huyu alikuwa kafiri. Hapa kuna dalili ya kujuzu kumtumia kafiri ili ustafidi kwa uzowefu wake. Anatufanyia kazi na sisi tunampa malipo yake. Hili ni mfano wa kufanya nao biashara katika mambo ya kimanufaa tunayoyahitajia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 165-166
  • Imechapishwa: 04/03/2019