129. Masuala yanayohusiana na kufanya biashara na makafiri

Suala la tatu: Kufanya muamala wa kidunia pamoja na makafiri katika kubadilishana mambo ya biashara na mambo ya manufaa. Hili ni jambo linaloruhusu. Waislamu hawakuacha kubadilisha bidhaa pamoja na makafiri, tokea zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakinunua kutoka kwa makafiri silaha na nyenginezo. Hili haliingii katika kujenga nao urafiki na kuwapenda. Huku ni kubadilishana nao mambo yenye manufaa. Maslahi yanarudi kwa waislamu. Halihusiani na kuwapenda. Bali hii ni biashara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 165
  • Imechapishwa: 04/03/2019