363 – Abu ´Uthmaan amesema:
“Nilikuwa na Salmaan (Radhiya Allaahu ´anh) chini ya mti. Akashika tawi lililokauka na kulitikisa, mpaka majani yake yakaanguka chini. Kisha akasema: “Ee Abu ´Uthmaan, huniulizi ni kwa nini nimefanya hivi?” Nikasema: “Ni kwa nini umefanya hivi?” Akasema: “Namna hiyo ndivo alifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nilipokuwa naye chini ya mti. Akashika tawi lililokauka na kulitikisa, mpaka majani yake yakaanguka chini. Kisha akasema: “Ee Salmaan, huniulizi ni kwa nini nimefanya hivi?” Nikasema: “Ni kwa nini umefanya hivi?” Akasema: “Hakika muislamu anapotawadha na akafanya vizuri wudhuu´ wake, kisha akaswali swalah zake tano, yanadondoka makosa yake kama yanavyodondoka majani haya.” Kisha akasoma:
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ
”Simamisha swalah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu – haya ni ukumbusho kwa wenye kukumbuka.”[1][2]
Ameipokea Ahmad, an-Nasaa’iy na at-Twabaraaniy. Wapokezi wote wa Ahmad wanatumiwa kama hoja katika Swahiyh upkezi wa kwanza Iispokuwa tu ´Aliy bin Zayd.
[1] 11:114
[2] Nzuri kupitia zingine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/268)
- Imechapishwa: 21/08/2023
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)