Maneno kukariri ndani ya Qur-aan

al-Haakim amesema: Nimemsikia pia Muhammad bin Ahmad bin Baaluuyah akisema: Jag Nimemsikia Ibn Khuzaymah akisema:

”Wale wajinga wanaodai kuwa Allaah hakariri maneno hawafahamu Kitabu cha Allaah. Allaah  amekariri maeneo mengi kuwa amemuumba Aadam. Amekariri kumtaja Muusa. Maeneo mengi, na kwa kukariri, amejihimidi Mwenyewe:

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

”Basi ni zipi katika neema za Mola wenu mnazikadhibisha?”[1]

Siwezi kudhani kuwa kuna muislamu anayefikiria kuwa Allaah halikariri jambo mara mbili. Hivo ndivo wanavosema wale wanaodai kuwa Qur-aan ni kiumbe. Wanafikiri kuwa ni jambo lisilowezekana kusema kuwa Allaah amekiumba kitu mara mbili.”

[1] 55:13

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/380)
  • Imechapishwa: 21/08/2023