Imethibiti katika Hadiyth kuwa watu pia watapimwa. Kama mfano wa Hadiyth isemayo:
“Hakika siku ya Qiyaamah ataletwa mtu mkubwa na mnene na hatokuwa na uzito mbele ya Allaah sawa na ubawa wa mbu.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu muundi wa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh):
“Hakika [miundi yake] ni yenye uzito zaidi kwenye mizani kuliko ya mmoja wenu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (4729) na Muslim (2785).
[2] Ahmad katika ”Musnad” yake (3991).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 20
- Imechapishwa: 25/04/2023