11. Msingi wa tano ambao ni kuamni siku ya Mwisho

Ni kuamini kwa kukata na kusadikisha siku ya Qiyaamah na yale yatayokuwa siku hiyo ikiwa ni pamoja na kufufuliwa, hesabu na malipo. Ni jambo limekusanya:

1 – Kuamini kufufuliwa kwa viwiliwili kutoka ndani ya makaburi na kuvirudishia roho. Ambaye hayaamini hayo ni kafiri. Amesema (Ta´ala):

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: “Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu! Bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale yote mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.”[1]

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ ۖ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

”Na wale waliokufuru wakasema: ”Saa haitotufikia.” Sema: ”Bila shaka! Naapa kwa Mola wangu itakufikieni, mjuzi wa mambo yaliyofichikana; hakuna kinachofichikana Kwake ingawa chenye uzito wa chembe mbinguni wala ardhini na wala kidogo zaidi kuliko hicho na wala kikubwa zaidi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.”[2]

وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ

”Wanakuuliza: ”Je, hayo ni kweli?” Sema: ”Ndio, naapa kwa Mola wangu! Hakika hayo bila shaka ni kweli nanyi si wenye kushinda.”[3]

2 – Kuamini hesabu. Amesema (Ta´ala):

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا

“Basi ama yule atakayepewa Kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi huyo atahesabiwa hesabu nyepesi na atageuka kwa familia yake hali ya kuwa ni mwenye furaha. Na ama yule atakayepewa Kitabu chake nyuma ya mgongo wake, basi huyo ataomba kuteketea.”[4]

3 – Kuamini kupewa kwa vitabu na madaftari ya matendo ima kwa upande wa kulia au upande wa kushoto. Amesema (Ta´ala):

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهِْ

“Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: “Hebu chukueni someni kitabu changu… “

mpaka aliposema:

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ

“Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: “Ee, laiti nisingelipewa kitabu changu.”[5]

4 – Kuamini kupimwa kwa matendo na watu kwenye mizani yenye kuhisiwa ambayo ina masahani mawili. Amesema (Ta´ala):

وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ

“Na mizani siku hiyo itakuwa ni haki. Basi ambao mizani yao itakuwa nzito – hao ndio watakaofaulu, na ambao mizani yao itakuwa khafifu – basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhulma Aayah Zetu.”[6]

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ نَارٌ حَامِيَةٌ

“Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito, basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake ni Haawiyah. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Haawiyah? Ni moto mkali mno wa mwako!”[7]

فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ , وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

”Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao, watakuwa katika [Moto wa] Jahannam wenye kudumishwa.”[8]

[1] 64:07

[2] 34:03

[3] 10:53

[4] 84:07-11

[5] 69:19-20

[6] 07:08-09

[7] 101:06-11

[8] 23:102-103

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 25/04/2023