117. Inatakiwa kuacha mijadala na uzushi

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Mizozo na mijadala katika dini inatakiwa kuachwa. Pia inatakiwa kuacha yale yote yaliyozuliwa na wazushi.

MAELEZO

Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuacha mizozo na mijadala. Lengo ni kutafuta haki. Ama kujadili, kupoteza wakati na kuweka nguvu zetu katika mijadala isiyozalisha matunda yoyote na kutaka maoni mbalimbli ya watu ndio yashinde ni jambo linalodhuru na halinufaishi kitu. Katika dini hakuna mivutano wala mijadala. Dini ni Qur-aan na Sunnah, na wala hakuna tofauti, mizozo wala mijadala. Hakuna kitu kinachoweza kutokomeza mambo hayo isipokuwa Qur-aan na Sunnah na wala hakuna awezaye kunufaika kwa Qur-aan na Sunnah isipokuwa wanachuoni. Ndio maana inatakiwa kurejea kwao.

Maoni, matendo na imani zote zilizozuliwa na wazushi baada ya Salaf na wakati huohuo yakawa yanaenda kinyume na Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf ni lazima kuyaacha. Yule mwenye kufanya kosa na akarudi katika msitari wa sawa haitakiwi kumsimanga; kinyume chake hiyo ni utukufu. Kurejea katika haki ni utukufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 07/09/2021