Swali: Je, wanalazimika wanawake walio na damu ya uzazi kutotoka nyumbani kabla ya kumalizika kwa muda?

Jibu: Mwanamke mwenye damu ya uzazi ni kama wanawake wengineo. Hapana vibaya kwake kutoka nje ya nyumbani kwake kukiwa kuna haja. Asipokuwa na haja basi bora kwa wanawake wote ni kutulizana nyumbani. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَى

“Tulizaneni majumbani mwenu na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa zama za ujahili.”[1]

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/226)
  • Imechapishwa: 07/09/2021