Damu ya uzazi haina kikomo kidogo

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke mwenye damu ya uzazi kuswali na kufunga akisafika kabla ya siku arobaini?

Jibu: Akisafika mwanamke mwenye damu ya uzazi kabla ya siku arobaini basi ni lazima kwake kuoga na baadaye aswali na kufunga Ramadhaan. Aidha ni halali kwa mume wake kumjamii kwa maafikiano ya wanazuoni. Damu ya uzazi haina kikomo kidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/255)
  • Imechapishwa: 07/09/2021