Abul-Faraj bin al-Jawziy amesema:

“Misiba inatibiwa kwa njia saba:

1- Mtu ajue kuwa dunia ni mahali pa majaribio na matatizo.

2- Mtu ajue kuwa misiba ndio uhakika wa mambo.

3- Mtu aufikirie msiba ulio mkubwa zaidi.

4- Mtu aangalie wale waliopatwa na misiba mfano wake.

5- Mtu aangalie waliosibiwa kwa msiba mbaya zaidi. Linamfanya mtu kuuchukulia mwepesi msiba wake.

6- Mtu kutarajia kupata kilicho bora zaidi ikiwa kuna uwezekano, kama mfano wa mtoto na mke. Kulisemwa kuambiwa Luqmaan: “Je, mke wako amefariki?” Akajibu: “Kuna mke mwingine amelala kitandani.”

7- Mtu ajibidishe kupata thawabu juu ya fadhila za subira na thawabu za wale wenye kusubiri na wenye kufurahia subira yao. Ikiwa ataongezea juu yake kuridhia msiba huo, haya ndio malengo timilifu yenye kufikiwa.”

Halafu mtu anaweza kuongezea juu yake mambo yafuatayo:

8- Mtu atambue kuwa vyovyote makadirio yalivyo basi ni kheri kwa mja.

9- Mtu atambue kuwa mitihani mizito inawapata tu wale walio bora.

10- Mtu atambue kuwa ni mtumwa na mtumwa hana kipingamizi chochote.

11- Mtu atambue kuwa yaliyopitika yamepitika kutokana na ridhaa ya Mmiliki na hivyo ni wajibu kwa mja kuridhia yale Mmiliki Aliyoridhia.

12- Mtu aikataze nafsi yake pale anapoanza kusononeka na kuona kuwa msiba ilikuwa ni lazima utokee. Hakuna faida yoyote ya kusononeka kwa kitu ambacho ilikuwa ni lazima kitokee.

13- Mtu atambue kuwa ni kwa muda mfupi tu kana kwamba hakukupitika kitu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 13/10/2016