Ibn-ul-Jawziy amesema:

“Lau dunia hii isingelikuwa ni mahali pa majaribio basi isingelichafua maradhi na uchafu na Mitume na waja wema wasingepatwa na matatizo.”

Aadam alipatwa na matatizo mpaka alipoiacha dunia hii.

Nuuh alilia miaka 300.

Ibraahiym alitupwa ndani ya moto na alikuwa amchinje mtoto wake.

Ya´quub alilia mpaka macho yake yakapofoka.

Muusa alikabiliwa na moyo msusuwavu wa Fir´awn na mitihani ya watu wake.

´Iysaa hakuweza isipokuwa kuishi katika jangwa na na katika hali ya umasikini.

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alistahamili ufakiri, ami yake Hamzah akauawa, ambaye alikuwa ni mmoja katika ndugu zake aliyekuwa anampenda sana, na watu wake wakamkata.

Hali kadhalika inahusiana na Mitume wengine na waja wema. Lau dunia hii ingelikuwa ni sehemu ya starehe basi muumini asingelikuwa na lolote la kufanya hapa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dunia ni jela la muumini na Pepo ya kafiri.” Ahmad, Muslim, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah.

Mambo yakishakuwa wazi namna hii ya kwamba dunia hii ni ya mitihani, jela na matatizo, basi mtu asikate kupatikana kwa misiba ndani yake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 23
  • Imechapishwa: 13/10/2016