Pindi msiba unapompata mtu, mali yake au mtoto wake, basi mja anatakiwa kutambua kuwa vyote hivyo vimepitika kwa Mmiliki na Muumbaji kuridhia. Kwa hivyo ni wajibu kwa mja kuridhia yale Mola aliyoridhia. Vilevile anatakiwa kukemea mwenendo wake na kujiambia:

“Hivi ulikuwa unajua kuwa haya yalikuwa si yenye kuepukwa? Kwa nini unasononeka? Ni jambo tu la muda mfupi. Litaenda kama vile halikupitika.”

Mwenye kuona malengo basi kuchukulia usahali uchungu wa dawa – na Allaha ndiye mwenye muwafikishaji.

Baadhi ya Salaf wamesema:

“Nimeona jinsi watu wengi wanavyosononeka kwa kuvuka mipaka pindi kunapotokea msiba. Ni kama kwamba walikuwa hawajui kuwa dunia hii imeumbwa kwa sababu ya lengo hilo. Je, aliye na afya huona kingine zaidi ya maradhi? Je, mtumzima huona kingine zaidi ya uzee? Je, aliyepo huona kingine zaidi ya kisichokuwepo?

Msiba wenyewe hautakiwi kukataliwa. Ni jambo la kimaumbile. Kinachokataliwa ni kuhuzunika kwa kupitiliza na kuchana nguo, kupiga mashavu na kuwa na kipingamizi juu ya Qadar. Mambo haya hayakirudisha kile kilichokosekana. Kinyume chake ni jambo linaonesha udhafi wa yule msononekaji na ni jambo pia linalopelekea katika adhabu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 13/10/2016