Msibiwaji anatakiwa kutambua kuwa lau kusingekuwepo mitihani na misiba katika dunia hii basi mja angelikuwa na kiburi, kujiona, dhuluma na moyo msusuwavu ambao ungesababisha maagamivu duniani na Aakhirah. Ni miongoni mwa huruma wa Mwingi wa huruma kupanga misiba mbalimbali yenye kumlinda mja na maradhi yake na kulinda ´ibaadah zake sahihi na kumsafisha na mambo mabaya yenye kuagamiza. Utakasifu wa kasoro ni wa Yule ambaye anarehemu kwa majaribio Yake na kutoa mitihani kwa neema Zake!

Lau Allaah asingeliwakabili waja Wake kwa mitihani na matatizo basi wangelikuwa wadhulumaji na wenye kutisha katika ardhi na wangelieneza ufisadi juu yake. Mwanaadamu ameumbwa namna hiyo kwamba anakuwa muasi lau hatoamrishwa na kukatazwa, afya nzuri na yuko na muda huru, pamoja na kuwa anajua ilivyokuwa kwa karne zilizotangulia. Mtu asemeje endapo ataghafilika nayo?

Kama Allaah anamtakia mja Wake mema basi humjaribu kutegemea na hali ya mja mwenyewe ili kumtoa yale maradhi yenye kuua. Pale anapomsafisha, basi humwacha akawa katika kile kiwango bora katika dunia hii, ambacho ni kumuabudu Allaah, kumpa mavazi mazuri kabisa huko Aakhirah, ambayo ni kumuona Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 25
  • Imechapishwa: 13/10/2016