Kuna khatari mfanya ´ibaadah mjinga wakati wa msiba akafanya mambo ambayo ni mabaya kuyaona na kuyasikia, kwa mfano kuwa na kipingamizi juu ya Qadar. Ni kwa sababu ni mwenye kujishughulisha na ´ibaadah zake. Watu wengi wa dini na waja wema hufanya mambo mabaya pindi watu wao wa karibu na wapenzi wao wanapofariki. Baadhi huchana nguo zao. Wengine hujipiga kwenye mashavu. Wengine wanakuwa na kipingamizi na Qadar. Ibn-ul-Jawziy amesema:

“Nilimwona mzee mmoja anayejulikana ambaye alikuwa karibu miaka 80. Alikuwa ni miongoni mwa watu wa dini ambaye siku zote anaswali katika mkusanyiko. Wakati msichana wake alipofariki akasema: “Kuswali haisaidii kitu. Hata ukiswali huitikiwi.” Alisema vilevile: “Kama sisi sio wenye kukataa basi Anawachukua watoto wetu wote.” Ndipo nikajua kuwa alikuwa anaswali na kufanya matendo mema kimila na sio kwa ujuzu na kuamini. Watu hawa wanamuabudu Allaah kwa mpaka.”

Baada ya hapo Ibn-ul-Jawziy akasema:

“Mjomba wangu Muhammad bin ´Uthmaan amenieleza alivyosikia namna kunavyozungumziwa juu ya mtu aliyekuwa na miaka 80 ambaye alikuwa haswali baada ya kuswali sana na kufanya matendo mema mengi. Akaacha yote hayo. Akamwita na kumwambia: “Mzee! Kwa nini huswali?” Akasema: “Vipi nitaswali ilihali wanangu wote wamefariki?” Kuanzia sasa sintoswalia Rakaa´ hata moja.” Akamshika na kutembelea nae ndani ya mji huo. Baada ya hapo akawa ni mwenye kuswali kila siku.”

Hakuna kitu kilicho na manufaa kabisa kama elimu. Mwanachuoni akikosa utulivu na kutokuwa na uvumilivu wakati wa msiba, anatambua kuwa ni kosa lake yeye na hivyo hujua namna atavyopumua. Kuhusu mfanya ´ibaadah mjinga kila anapotumbukia kwa chini hudhania kuwa anaenda juu. Ndio maana inatakiwa kwa mtu kujitibu kwa dawa za Kishari´ah wakati anapopatwa na msiba. Kuna methali inayosema:

“Wakati wa mitihani mtu anakuwa ima ni mwenye kutukuzwa au kufedheheshwa.”

Je, mtu hajui kuwa ni lazima aitenge dunia hii? Tunaomba kinga kwa Allaah kutokana na ukosevu wa subira wakati wa mitihani. Tunamuomba uthabiti katika jambo hili. Mtu anaishi katika hali ya khatari ikiwa yuko na kipingamizi juu ya Qadar. Tunamuomba Allaah mwisho mwema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 13/10/2016