16. Msiba unatakiwa kuwa na ´ibaadah badala ya vilio na malalamiko

Yule ambaye amepewa msiba au amepewa msiba mtoto wake au mwengine anatakiwa katika kipindi cha maradhi yake kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jall), kuomba msamaha na kufanya ´ibaadah. Salaf walikuwa wakichukia kuwashtakia/kuwalalamikia viumbe. Hata kama ni jambo linaweza kuwepesisha kidogo linaonyesha udhaifu wa mtu. Kusubiri na kutofanya hivo kunaonyesha nguvu na ukakamavu. Linaeneza hekima ya Allaah kwa mja na huruma wa rafiki na kumuathiri adui anayefurahikia mahuzuniko ya mtu.

Ibn Abiy Dunyaa amepokea kuwa Ismaa´iyl amesema:

“Tulimtembelea Warqaa´ bin ´Umar pindi alipokuwa anataka kukata roho. Akasema: “Laa ilaaha illa Allaah” na “Allaahu Akbar” na kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jall). Watu wakamtembelea na kumsalimia na yeye akawaitikia. Watu walipokithiri akamwambia mwanaye: “Ee mwanangu! Nifanye nisiwaitikie watu hawa. Nifanye wasinisumbue pindi niko namdhukuru Mola wangu (´Azza wa Jall).”

Abu Muhammad al-Hariyriy amesema:

“Nilikuwa kwa al-Junayd masaa mawili kabla ya kufa. Hakuacha kuendelea kusoma Qur-aan na kuswali. Nikamwambia: “Abul-Qaasim! Wewe si uko katika hali ngumu!” Akasema: “Ee Abu Muhammad! Muda huu ndio nina haja zaidi nao.” Akaendelea kufanya hivo mpaka alipoiacha dunia hii.

Imepokelewa ya kwamba Ibliys ndiye mbaya zaidi kwa mwanaadamu kabla hajakata roho. Huwaambia wasaidizi wake: “Mwandameni! Mkimkosa hivi sasa ndio hamtompata tena.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 27
  • Imechapishwa: 13/10/2016