Haki zao kwa Ummah ni miongoni mwa haki kuu. Wana juu ya Ummah haki zifuatazo:
1 – Kuwapenda kwa moyo na kuwasifu kwa mdomo kutokana na waliyoyafanya katika wema na ihsaan.
2 – Kuwatakia rehema na kuwaombea msamaha kwa ajili ya kuhakikisha maneno Yake (Ta´ala):
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Na wale waliokuja baada yao ni wenye kusema: “Mola wetu!Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini – Mola wetu! Hakika ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.”[1]
3 – Kunyamazia mapungufu yao yaliyotokea kwa mmoja katika wao. Ni machache yakilinganishwa na mazuri na ubora wao. Isitoshe pengine yametokana na ijtihaad yenye kusamehewa na matendo ambayo mtu anapewa udhuru kwayo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msiwatukane Maswahabah wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi Mwake lau mmoja wenu atajitolea dhahabu mfano wa mlima wa Uhud basi hatofikia viganja viwili vya mikono vilivyojazwa na mmoja wao wala nusu yake.”[2]
Kuna maafikiano juu yake.
[1] 48:10
[2] al-Bukhaariy (3673) na Muslim (2541, 222).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 151
- Imechapishwa: 16/12/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)