Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwatukane Maswahabah wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi Mwake lau mmoja wenu atajitolea dhahabu mfano wa mlima wa Uhud basi hatofikia viganja viwili vya mikono vilivyojazwa na mmoja wao wala nusu yake.”[1]

MAELEZO

Kuna sampuli tatu za kuwatukana Maswahabah:

1 – Kuwatukana kwa yale yanayopelekea kuwakufurisha wengi wao au kwamba wengi wao ni mafusaki. Huu ni ukafiri. Kwa sababu anamkadhibisha Allaah na Mtume Wake kwa kule kuwasifu na kuwawia radhi. Bali mwenye mashaka juu ya ukafiri wa mtu kama huyu basi ukafiri wake ni kwa dhati yake kabisa. Kwani maneno haya maana yake ni kwamba walionakili Qur-aan na Sunnah ni makafiri au watenda maovu wakubwa.

2 – Akawatukana kwa kuwalaani na kuwafedhehesha. Wanazuoni wana maoni mawili juu ya hilo. Maoni yanayosema kuwa hakufuru wanaona kuwa ni lazima apigwe bakora au afungwe jela mpaka afe au ajirejee kutokana na aliyoyasema.

3 – Akawatukana kwa mambo yasiyoitia dosari dini yao. Kwa mfano kwamba ni mabakhili au waoga. Hakufurishwi. Hata hivyo anatakiwa kuadhibiwa kwa mambo yatayomzuia kutokamana na mambo hayo. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ametaja maana ya haya katika kitabu “Swaarim-ul-Mas-luul” na imenukuliwa kutoka kwa Ahmad, katika ukurasa wa 573, ambapo amesema:

“Haijuzu kwa yeyote kutaja chochote katika mabaya yao wala asimshambulie yeyote katika wao kwa kasoro au upungufu. Atakayefanya hivo anatakiwa kutiwa adabu. Akitubu ni sawa na vinginevyo achapwe viboko mpaka afe au ajirejee.”

[1] al-Bukhaariy (3673) na Muslim (2541, 222).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 16/12/2022