110. Haki za wakeze Mtume (صلى الله عليه وسلم)

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Katika Sunnah ni kuwatakia radhi wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakika wao ndio mama wa waumini watwahirifu na wako mbali kabisa na kila chafu. Mbora wao ni Khadiyjah bint Khuwaylid na ´Aaishah asw-Swiddiyqah bint asw-Swiddiyq ambaye Allaah amemtakasa katika Kitabu Chake. Ni mke wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) duniani na Aakhirah. Yeyote atayemshutumu kwa yale Allaah aliyomtakasa, basi atakuwa amemkufuru Allaah Mtukutu.

MAELEZO

Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wakeze duniani na Aakhirah na ni mama wa waumini. Wana heshima na matukuzo yanayolingana naye kama wakeze Mtume wa mwisho. Ni watu wa nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wasafi na wenye kusafishwa, wazuri na waliofanywa wazuri, wenye kujitakasa na uchafu na wenye kutakaswa na kila uovu unaotia dosari katika heshima na magodoro yao. Wanawake wazuri ni wa wanamme wazuri na wanamme wazuri ni wa wanawake wazuri. Allaah awaridhie wote nao wote wamuie radhi na swalah na salamu zimwendee Mtume Wake mkweli na mwaminifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 152-153
  • Imechapishwa: 16/12/2022