106. Uislamu uko kati na kati kuhusiana na jambo la usafi

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

”Hadiyth hii inafahamisha wingi wa yale ambayo Allaah amemuwekea Shari´ah Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kutofautiana na mayahudi na wingi wa namna (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyojitofautisha nao. Mpaka wakafikia kusema:

”Bwana huyu anachotaka ni yeye kujitofautisha nasi katika kila kitu.”

Wakati fulani kujitafautisha kunakuwa katika hukumu yenyewe, wakati mwingine katika mbinu zenyewe. Kuhusu kumwepuka mwanamke aliye ndani ya hedhi hakuhusiani na hukumu yenyewe, bali mbinu zake kwa sababu Allaah ameweka Shari´ah ya kumkaribia mwenye hedhi muda wa kuwa mtu ataepuka tupu yake. Wakati baadhi ya Maswahabah walipotaka kuongeza kujitofautisha kwa njia ya kuacha yale yaliyowekwa katika Shari´ah na Allaah, ukabadilika uso wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mlango huu unahusiana na usafi, jambo ambalo mayahudi walikuwa na uhusiano mgumu sana nalo. Matokeo yake manaswara wakazua kuyaacha yote hayo kwa kiasi cha kwamba wakaona chochote kinachokuwa najisi – mtazamo huo usiokuwa na dalili kutoka kwa Allaah. Basi Allaah akauongoza ummah wa kati na kati katika yale yaliyo kati na kati katika jambo hilo. Ingawa msimamo uliokuwa umechukuliwa na mayahudi ulikuwa umewekwa katika Shari´ah kipindi fulani, kujiepusha na yale ambayo hayakuwekwa na Allaah katika Shari´ah ni kujifananisha na mayahudi, na kuyafanya yale ambayo Allaah amefanya yaepukwe ni kujifananisha na manaswara. Uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Tazama “Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 166
  • Imechapishwa: 30/10/2023