107. Adhaana ni katika mambo ya Uislamu na waislamu

Kuhusu Sunnah, zipo dalili nyingi na nzuri zinazotilia nguvu kanuni iliyotangulia. Isitoshe hazikomeki na kitendo kimoja isipokuwa zinaenea katika vipengele vingine vilivyowekwa katika Shari´ah, kukiwemo usafi, swalah na mengine mengi. Ni ubainifu na upambanuzi wa yale yaliyotajwa kwa jumla katika Aayah za Qur-aan zilizotangulia juu ya suala hili. Hapa nakutajia nazo ili uwe juu ya ubainifu wa yale niliyoyasema…

Swalah:

1 – Abu ´Umar bin Anas amesimulia kutoka kwa mmoja katika ami zake wa ki-Answaar amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitafakari ni namna gani atawaita watu katika swalah ambapo akaambiwa: ”Simamisha bendera unapofika wakati wa swalah. Watu watakapoiona basi wataelezana.” Haikumpendeza. Ndipo kukatajwa pembe ya mayahudi. Haikumpendeza na akasema: ”Ni katika mambo ya mayahudi.” Ndipo kukatajwa kengele ya mnara ambapo akasema: ”Ni katika mambo ya manaswara.” ´Abdullaah bin Zayd bin ´Abdi Rabbih, ambaye aliguswa na jambo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akaondoka na akaota adhaana usingizini mwake.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh na nimeitaja katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (511). Huko nimetaja wale maimamu walioisahihisha. Makusudio ya Hadiyth yako wazi kabisa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 167
  • Imechapishwa: 30/10/2023