Dhikr iliyowekwa katika Shari´ah baada ya Fajr

Swali: Je, kusema ´Subhaan Allaah` baada ya Fajr mpaka kuchomoza kwa jua, kama ilivyokuja katika Aayah, ndio bora au kusoma Qur-aan? Ni upi wakati bora wa kuhifadhi Qur-aan?

Jibu: Bora ni kutilia umuhimu kusema ´Subhaan Allaah` na Adhkaar zilizowekwa katika Shari´ah. Lengo ni aifanye kila ´ibaadah ndani ya wakati wake mwishoni mwa mchana, mwanzoni mwa usiku au mwanzoni mwa asubuhi. Bora ni kutilia umuhimu Adhkaar na du´aa zilizowekwa katika Shari´ah. Ni sawa pia akisoma Qur-aan. Lakini akisoma Adhkaar zilizowekwa katika Shari´ah ni sawa kwa njia ya kwamba kila kitu akakiweka mahali pake. Kwa mfano katika Rukuu´ anatakiwa kusema:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

na asiombe du´aa. Aseme:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

Atapoinuka aseme:

سبحانك اللهم ربنا و وبحمدك,اللهم اغفر لي

“Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote unastahiki Wewe. Ee Allaah! Nisamehe!”

Baina ya Sujuud mbili aombe kwa kusema:

ربي اغفر لي، ربي اغفر لي

 “Mola wangu nisamehe. Mola wangu nisamehe.”

Kila kitu akiweke mahali pake, ndio jambo lililowekwa katika Shari´ah. Akiomba du´aa kwa wingi, akasema ´Subhaan Allaah` kwa wingi, akasema ´Laa ilaaha illa Allaah` kwa wingi, akamtukuza Allaah na akakithirithisha du´aa zilizowekwa katika Shari´ah mida ya asubuhi na jioni ndio bora. Akisoma Qur-aan yote ni kheri tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23057/هل-التسبيح-بعد-الفجر-افضل-ام-التلاوة
  • Imechapishwa: 30/10/2023