Malaika wengine wamepewa kazi ya kumlinda mwanadamu asifikwe na majanga na kushambuliwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ

“Ana Malaika wanaofuatana kwa zamu mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa amri ya Allaah.”[1]

Wanamuhifadhi mtu kwa amri ya Allaah mpaka pale yatapomfika makadirio ya Allaah; basi kipindi hicho wanamwacha na matokeo yake anafikwa na yale aliyompangia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo mtu anaweza kufikwa na hali ya khatari kabisa lakini hata hivyo akasalimika, kwa sababu yuko pamoja naye Malaika wanaomuhifadhi kutokana na amri ya Allaah (´Azza wa Jall). Hawa ndio Malaika wanaofuatana.

[1] 13:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 80
  • Imechapishwa: 31/08/2021