105. Malaika wa kifo na wasaidizi wake

Wako Malaika wengine ambao kazi yao ni kuzitoa roho za viumbe. Kiongozi wao ni Malaika wa kifo. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ

“Sema: “Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Mola wenu mtarejeshwa.”[1]

Anakuwa na Malaika wasaidizi wengine wanaotoa roho nje kutoka kwenye kiwiliwili. Pindi wote wanapokusanyika ndipo Malaika wa kifo anaichukua. Amesema (Ta´ala):

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ

“Naye ndiye anayekufisheni usiku na anajua yale myafanyayo mchana halafu anakufufueni humo ili utimizwe muda maalum uliokadiriwa. Kisha Kwake pekee ni marejeo yenu, kisha atakujulisheni kuhusu yale mliyokuwa mkiyatenda. Naye ni Mkuu kabisa asiyeshindika juu ya waja Wake na anakutumieni Malaika wanaohifadhi mpaka kinapomfikia mmoja wenu kifo, basi wajumbe Wetu humfisha, nao hawazembei.”[2]

Bi maana Malaika.

[1] 32:11

[2] 6:61

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 31/08/2021