Mtoto anatakiwa kuzinduliwa makosa ya ´Aqiydah masomoni

Swali: Ni lipi la wajibu kwa mwalimu anayepata kosa katika silebasi ya masomo? Je, awabainishie wanafunzi au aruke somo hilo? Mwelekezaji amesema kuwa asiruke kitu chochote na asiwabainishie kosa lolote wanafunzi. Anachomaanisha badala yake kosa lipelekewe katika wizara.

Jibu: Ikiwa katika silebasi ya masomo kuna kitu kinachoenda kinyume na ijtihaad yake, basi asibadilishe. Hujui usawa uko kwako au kwa yule mwengine. Wewe sio Mtume ambaye unateremshiwa Wahy mpaka useme kuwa maoni yako ndio ya sawa na ya mwengine ni ya makosa. Wewe ni mwenye kujitahidi peke yake; kuna uwezekano usawa uko pamoja nawe au umekosea. Kwa hivyo usibadilishe chochote.

Ikiwa suala hilo halikubali mambo ya ijtihaad, kukiwemo mambo ya ´Aqiydah, basi ni lazima uwabainishie. Lakini haitoshi kuwabainishia wanafunzi. Ni lazima uwaandikie wale wasimamizi katika wizara. Ikiwa halikufua dafu, basi waandikie wanazuoni. Hapa ni pale ambapo suala linahusiana na ´Aqiydah. Mfano wa kosa hilo ni pale ambapo kutakuwa kumeandikwa kwamba Allaah ameumba Qur-aan na kwamba haikuteremsha. Hili haifai kulikubali. Hata hivyo sifikirii kwamba chekechea kuna silebasi inayokwenda kinyume na ´Aqiydah ya Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (18 B)
  • Imechapishwa: 31/08/2021